TuneCore, kampuni inayoongoza ya usambazaji wa muziki wa kidijitali na kukusanya mirabaha ya wasanii huru, imezindua shughuli zake barani Afrika. Jade Leaf ameajiriwa kama Mkuu wa TuneCore wa Afrika ya Kusini na atashiriki majukumu ya nchi kuu zilizo Afrika Mashariki na Chioma Onuchukwu, ambaye ameajiriwa kama Mkuu wa TuneCore wa Afrika Magharibi. Leaf na Onuchukwu wataripoti kwa Faryal Khan-Thompson, Makamu wa Rais wa Kimataifa katika TuneCore.
Onuchukwu atakuwa Nijeria na atasimamia nchi zilizomo Afrika Magharibi ikiwemo Nijeria, Ghana, Liberia, Siera Leoni na Gambia. Atasimamia pia Tanzania na Ethiopia zilizomo Afrika Mashariki. Himaya ya Leaf inajumuisha Afrika ya Kusini, ikiwemo Afrika Kusini, ambayo itakuwa makao yake makuu, na hata pia Namibia, Botswana, Zimbabwe, Zambia, Malawi na Lesotho. Leaf atasimamia pia shughuli za TuneCore katika nchi za Afrika Mashariki, Kenya na Uganda.
“Ninafuraha kuwa ninajiunga na kampuni huru maarufu ya usambazaji wa muziki, hasa katika karne hii ya ajabu sana kwa wabunifu wa muziki barani Afrika wakati ambao tunapata kutambuliwa kimataifa na tunaongezea bidii.” Alisema Onuchukwu. Ninatazamia kushirikiana na kuwaunga mkono wasanii wa nchini.”
Kabla ya kujiunga na TuneCore, Onuchukwu alikuwa Meneja wa Masoko katika uduX Music, jukwaa la kutiririsha muziki nchini Nijeria. Hapo alifanya kazi moja kwa moja na wasanii maarufu wa Afrika kama vile Davido, Yemi Alade, Patoranking, Kizz Daniel na wengine wengi.
“Ninafuraha sana kujiunga na timu hii wakati ambao mazungumzo ya kimataifa yanahusu uhuru na umiliki.” Alisema Leaf. TuneCore inafungua ulimwengu wa uwezo kwa wasanii huru katika kila ngazi ya kazi zao. Afrika ni makao ya wasanii mbalimbali wanaotafuta huduma thabiti ya usambazaji inayoelewa mahitaji yao ya nchini na inaweza kuwapa nafasi ya kubadilisha sanaa yao kuwa ufanisi wa kibiashara.”
Hapo awali, Leaf alifanya kazi katika kampuni kubwa zaidi Afrika ya TV ya kulipia, Multichoice kama Meneja wa Masoko wa Vituo vya Vijana na Muziki, ambapo aliongoza katika kuipa kampuni sura mpya na katika juhudi za masoko kwa Kituo kikubwa cha Muziki wa TV cha Channel O. Kabla ya hiyo, alifanya kazi Sony Music Entertainment Afrika, akilenga wasanii na maudhui ya Kiafrika, na hata pia kampeni nyingi za masoko na miradi ya wasanii wa nchini na wa kimataifa.
Kumekuwa na ongezeko la kukubalika kwa huduma za utiririshaji barani Afrika, ukuaji huu umesababishwa na mambo kadhaa kama vile kuongezeka kwa ufikiaji wa intaneti kupitia simu mahiri, kuingia kwa majukwaa ya utiririshaji ya kimataifa na ya nchini katika himaya kuu na idadi ya vijana – zaidi ya asilimia 60 ya Waafrika wamo chini ya umri wa miaka 25.
Katika mwaka wa 2020, TuneCore ilishuhudia ongezeko katika matoleo ya muziki kimataifa, huku wasanii wengi wa Kiafrika wakichagua kutumia Wasambazaji wa DIY – DJ Spinall na Small Doctor nchini Nigeria, Spoegwolf nchini Afrika Kusini, Mpho Sebina nchini Botswana na Fena Gitu nchini Kenya.
“Afrika ni soko linalosisimua sana la muziki lenye uwezo mkubwa wa kukua.” Alisema Khan-Thompson. Kwa kuwaajiri Jade na Chioma kuongoza juhudi zetu, TuneCore iko mahali pazuri pa kutumia nafasi hizi kwa wasanii huru katika bara hili. Chioma na Jade wanaleta tajiriba kubwa na shauku halisi ya kuwasaidia wasanii kufanya ndoto zao kuwa kweli. Ninafurahi zaidi kuwa na wanawake hawa wawili wa ajabu wakiwakilisha kampuni ya TuneCore katika bara hili”
TuneCore, inayomilikiwa na Believe ya Paris, imekuwa ikipanua kwa haraka shughuli zake za kimataifa, kuanzia nchi 5 mwaka wa 2020 hadi nchi 8 na maeneo 3 kuu katika mwaka wa 2021. Kampuni hii iliongezea India, Urusi na Brazili mwaka uliopita na mwaka huu ikaongezea LATAM, Asia ya Kusini mashariki na Afrika. Tovuti ya kampuni imejanibiwa kwa nchi 8 na ikatafsiriwa kwa lugha 13 na zinaendelea kukua.

FOR FAST LATEST UPDATES ON
AUDIOS, VIDEOS, MIXTAPES, FREE BEATS AND INSTRUMENTALS
CLICK HERE TO JOIN OUR WHATSAPP GROUP
