Home Music Mjue Msanii Allay Fabrizio, Mombasa Anajulikana Kama “Hazzard Classic”

Mjue Msanii Allay Fabrizio, Mombasa Anajulikana Kama “Hazzard Classic”

Leo ndani ya uwanja huu wa www.mzukakibao.com tutakula kitu laivu bila chenga kutoka kwa staa wa muziki wa Kizazi Kipya, Huyu si mwingine bali ni Allay Fabrizio.
Kabla ya kulisongesha jahazi mbele zaidi, Allay Fabrizio alizaliwa Mtwapa, jijini Mombasa. Kando na mziki Allay Fabrizio ni Animator, pia anamiliki Botique, Salon na Kinyozi chini lebo yake ya Hazzard Classic, Mtwapa.
Back to music, Allay Fabrizio kwa sasa yupo chini ya lebo ya Neptune Records, ambayo inamilikiwa na producer Lameckboy Kenya.

Moja juu ya moja pata kufahamu mengi kumhusu.

Mzuka Kibao: Majina yako kamili ni gani?

Allay Fabrizio: Majina kamili naitwa Ali Maulid na lakisanii najulikana kama Allay Fabrizio.

Mzuka Kibao: Hivi wacha ile time ulianza kuimba, serious music ulinza lini hasa?

Allay Fabrizo: Serious music nlianza mwaka Jana, kwa sababu muda wote nmekuwa nikisoma game.

Mzuka Kibao: Baada ya kusoma game, umefaulu kutoa vibao vingapi na je uko na lebel inakusukuma?

Allay Fabrizo: Kwa sasa niko na vibao vitatu, viwili nmefanya solo , 1:Nigande. 2:Faidika na chengine ni Party mood ambacho tulifanya wasanii wengi wa Neptune Recordz. Kwa upande wa management, producer wangu Lameckboy Kenya ndo amenishikilia na kunisapot.

Mzuka Kibao: Kama unavyoona wasanii ni wengi, je unaamini unavigezo vyakutawala airwaves?

Allay Fabrizio: Naam naamini sina kama iwapo watu watazipokea kazi zangu kwa uzuri na kuzisapot naamin ntaweza sana.

Mzuka Kibao: Unawaambiaje mafans wako kwa sasa kuhusiana na kazi zako?

Allay Fabrizio: Mafans nawambia watarajie kazi poa kutoka kwangu, na video zinakam na pia more good things, na big up producer wangu Lameckboy Kenya kwa sapot, na Hazzard Classic crew yangu mzima.

Mzuka Kibao: Asante sana kwa mdaa wako. Hivi Social media handle zako ni?

Allay Fabrizio:

Facebook : Allay Fabrizio

Twitter: @AllayFabrizio

YouTube: @Allay Fabrizio

Instagram: @FabrizioAllay

Angalia Picha zingine zake Allay Fabrizio

Previous articleMixtape | Dj Jones 254 – The World Mix (Vol.9)
Next articleRicc Berry Leaves Nicah The Queen For Phieso
DISCLAIMER: Mzukakibao.com do not claim ownership of any of the Songs and Videos that we upload and any copyright infringement complaints will be executed immediately! It is our policy to honor all take-down requests. Email: mzukakibao194@gmail.com Twitter: @mzukakibao Facebook: Mzuka Kibao Instagram: @mzukakibao

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here