Home News Alichokisema Katalang’ Kumhusu Nadia Mukami Kitakuacha Mdomo Wazi

Alichokisema Katalang’ Kumhusu Nadia Mukami Kitakuacha Mdomo Wazi

Hivi leo Mzuka Kibao imekutana na facebook post ya miaka miwili iliyopita ambapo Msanii wa Genge Lang’ Katalang’ kwa ufupi K’Lang anamtakia kila la heri msanii wa kike Nadia Mukami wakati huo ambapo walionyesha kuwa na ukaribu sana.

Picha hiyo ambayo inaonekana kupostiwa msimu wa Easter mwaka wa 2017 inadhihirisha wazi alivomweka katika maombi Nadia Mukami na ni kweli baadae akaja akatoka mwanadada huyo. Hivi ni kweli kwamba kuhit kwa Nadia ilitabiriwa?

Licha kubaki underground kwa muda mrefu Lang’ Katalang’ ameonyesha juhudi za kutaka kutoka ikiwemo kupatanishwa na wanahabari na wanaharakati mbalimbali humu nchini.

Kulingana na Katalang’ ambaye alimtangulia Nadia kuingia katika ulingo wa sanaa wakiwa Chuo Kikuu Cha Maseno anaamini kuwa wakati wake ndio bado haujafika wa kuhiti rasmi.

Ila baada ya kumhoji kuhusiana na picha hiyo ya Nadia, alisema kwamba ni baraka kuona watu ama wasanii walio karibu naye wakitimiza ndoto zao manake inadhihirisha hata siku yake yaja.

Kando na Nadia inasemekana Katalang’ aliwahi kutabiri kutoka kwake msanii wa Tanzania Rosa Ree ambaye amekuwa mshambulizi mkubwa kwenye historia ya rap Tanzania .Rosa Ree vilevile anafanya vizuri.

Nadia Mukami baada ya kufanya Kesi na Barua ya Siri akiwa bado underground amefanikiwa kuachia hit baada ya nyingine zikiwemo African Lover, Radio Love ft Arrowboy and Lola ft Masauti.

Rosa Ree Vilevile anawika na ngoma nyingi nzuri kama Kipopo na Banjuka.

Meanwhile Katalang’ ameachia video mpya inayoitwa Wagwan mwezi uliopita kisha pia akafanikiwa kurudia Collabo yake na Chege Chigunda ,Nataka Kuwa Nawe. Ngoma ambazo zipo YouTube.

♥️Thank you for Visiting www.mzukakibao.com

👍👍Welcome On Board👍👍

CLICK HERE TO JOIN OUR

WHATSAPP GROUP

You’ll Be the First To Get all Kenyan Latest Music.

☝️💯💯💯💯🔉🔉

FOR FAST LATEST UPDATES ON

AUDIOS, VIDEOS, MIXTAPES, FREE BEATS AND INSTRUMENTALS

CLICK HERE TO JOIN OUR WHATSAPP GROUP

🎵🎶🎹🎼🍗 💃 🎸🎧🔉

MZUKA KIBAO TELEGRAM CHANNEL

SUBSCRIBE TO STAY UPDATED

🎵🎵🎶🎵🎵🎤🎵🎵🎹

🎵 🎶 🎹 🎼 🍗 💃 🎸
Previous articleMusic: Mr. Jack – One by one | @mrjack1k
Next articleNew Music | Bluboi – Loke
DISCLAIMER: Mzukakibao.com do not claim ownership of any of the Songs and Videos that we upload and any copyright infringement complaints will be executed immediately! It is our policy to honor all take-down requests. Email: mzukakibao194@gmail.com Twitter: @mzukakibao Facebook: Mzuka Kibao Instagram: @mzukakibao