Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akizungumza mapema Siku ya leo mbele ya wageni waalikwa jijini Dar es Salaaam kabla ya uzinduzi rasmi wa mashindano makubwa ya vipaji kwa ukanda wa Africa Mashariki (East Africa’s Got Talent).

Mashindano hayo yanaendeshwa kwenye mabara mbalimbali huku takribani nchi 58 zikishiriki katika mashindano hayo.

Kwa mara ya kwanza katika Historia Clouds Media Group imepewa leseni kamili (Franchised) ya kuendesha shindano hilo la EAGT ambapo kwa Sasa mashindano hayo yatafanyika nchi nne ikiwemo Tanzania, Uganda, Rwanda na Kenya, na mshindi ataondoka na kitita cha shilingi Milioni 5 pesa za Kenya.

Hata hivyo Mkurugenzi Joseph Kusaga amewataka vijana wa kitanzania popote walipo kujitokeza kushiriki shindano hilo la kipekee kabisa.

4 COMMENTS

 1. My name is E point from kenya i am a gospel hiphop artist,
  I just love the whole idea of EAGT simply you promote all kind and type of talents around AFRICA
  I have sighnd up for the pre auditions and i cant wait to show the world what i realy have
  I love EAST AFRICA GOT TALENT
  I LOVE AFRICA
  +254704251596
  epointnofficiol.gmail.com

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

3 + 11 =