Home News COKE STUDIO AFRICA INATANGAZA ONYESHO LA WANAWAKE PEKEE KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE...

COKE STUDIO AFRICA INATANGAZA ONYESHO LA WANAWAKE PEKEE KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI AMBAPO ITAKUWA NDIO SEHEMU YA MWISHO

NDOVU NI KUU - KRISPAH X KHALIGRAPH JONES X BOUTROSS

Katika kuadhimisha na kusheherekea Siku ya Wanawake Duniani 2019, msimu wa Coke Studio Africa unatangaza ujio wa onyesho la wanawake pekee katika kauli yenye nguvu na njia ya mfano wa kuigwa. Hii itakuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya muziki wa Kiafrika kushirikisha wanawake wote kwenye onyesho, ambalo litajumuisha waimbaji wa kike, wakufoka, watayarishaji wa muziki, watengeneza muziki, kikundi kamili cha muziki, vile vile wafanyakazi wa muhimu wa nyuma ya pazia kama waongozaji wa maudhui, waandidhi wa miongozo, wahariri, waongozaji wa kamera na wakuu wa sakafu na wengine.

Kwa zaidi ya misimu sita ya Coke Studio Africa, kipindi hiki kimeendelea kuanika talanta na fursa kwa wanawake katika sanaa na kiwanda cha burudani kwa ujumla. Kwa sasa, takribani asilimia 60 ya wafanyakazi wenye uweledi ambao wanafanya kazi kwenye Coke Studio inaundwa na wanawake. Coke Studio itaendelea kutoa fursa zenye maana na zenye ushindani kwa wanawake kwenye uwanja wa sanaa na muziki, kupitia jukwaa lake.

Orodha ya wapiga vyombo wa juu zaidi kutoka Kenya ambao watakuwa sehemu ya Bendi ya Wanawake wote kwenye onyesho hili la mwisho la Coke Studio itawajumuisha: Kasiva Mutua (Mpiga Ngoma), Wendy Kemunto (Sauti), Ivy Alexander (Gitaa), Naomi Ziro (Gitaa la Besi) na Mutindi Tindi Muasa (Kinanda). Orodha ya waimbaji wa kike wa juu zaidi kutoka kona zote za bara la Afrika itawajumuisha wasanii wa Kenya: Nazizi na Nadia Mukami, Lioness (Namibia), Boity (Afrika Kusini), Sheebah (Uganda), Nandy (Tanzania), Mahlet (Ethiopia), Lourena Nhate (Msumbiji), Tamy (Zimbabwe) na mtayarishaji wa muziki Viola Karuri (Kenya) na wengine.


Monali Shah, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Maudhui wa Kampuni ya Coca-Cola kwa upande wa Kusini na Afrika Mashariki amesema, “Tunafuraha kutangaza sehemu ya mwisho ya Coke Studio Africa 2019 ambayo itajumuisha wanawake wote. Ni kwa mara ya kwanza kwa utayarishaji wa Coke Studio Africa kupiga hatua hii kubwa katika historia yake kwa kuangazia talanta au vipaji tulivyonavyo kwenye burudani. Aina ya vipaji na wasanii ambao tulikutana nao walikuwa wakuvutia zaidi kiasi cha kwamba tunashindwa kusubiri hadi mashabiki wa muziki katika kipindi chetu kujionea ukubwa wa onyesho hili ambalo litaruka katika mataifa 40 kuanzia Machi 29, 2019.

🎵 🎶 🎹 🎼 🍗 💃 🎸

SONG OF THE WEEK

V THE ALBUM By Brown Mauzo Utanizalia - BROWN MAUZO Moyo Wangu - BROWN MAUZO Yumba - Brown Mauzo × Masauti Naoa - Brown Mauzo Nipokee - Brown Mauzo My lover - Brown Mauzo × Mwasi Butterfly - Brown Mauzo Body - Brown Mauzo x Ndovu kuu Mawazo Remix - Brown Mauzo ft Baraka The Prince x kaa La Moto Wewe Tu - Brown Mauzo Moyo Wangu Accoustic - Brown Mauzo Dawa - Brown Mauzo ️💯💯

FOR FAST LATEST UPDATES ON

AUDIOS, VIDEOS, MIXTAPES, FREE BEATS AND INSTRUMENTALS

CLICK HERE TO JOIN OUR WHATSAPP GROUP

FRISKY By Maandy Mambo Gani - MAANDY Relax - MAANDY Shash Na Lipgloss - MAANDY MoneyBack Freestyle - MAANDY Magizani - MAANDY feat. BREEDER LW Bad Gal Anthem - MAANDY feat. FENA Forbidden Fruit - MAANDY Hivi Na Hivo - MAANDY Uongo - MAANDY Money Man - MAANDY Sirudi Home Remix - MAANDY feat. BREEDER LW & NDOVU KUU One Day - MAANDY

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here