Home Artistes Huyu Ndiye Msanii Wa Kike Anayetarajiwa Kutamba Mwaka Wa 2018 Coast Na...

Huyu Ndiye Msanii Wa Kike Anayetarajiwa Kutamba Mwaka Wa 2018 Coast Na Kenya Nzima

NDOVU NI KUU - KRISPAH X KHALIGRAPH JONES X BOUTROSS

Ukiwataja wasanii wa muziki wakike kutokea Pwani ya Kenya, basi wanaofahamika watakuwa ni Nyota Ndogo na Ari Loveness tu.

Grace Pendo Wanje almaarufu ARI LOVENESS ni msanii mchanga ambaye kama utausikiliza wimbo wake ‘You Are Mine’ utakubali bila ubishi kuwa muziki ni kipaji chake na halazimishi.

Wengi wamepata kumfahamu kupitia mikono ya producer Lameckboy Kenya na katika meza yetu tumefanya naye interview ili kumfahamu zaidi na hivi ndio akafunguka.

Mzuka kibao : Majina yako kamili na yakisanii ni?

Ari Loveness: Mi naitwa Grace Pendo Wanje, na lakisanii ni Ari Loveness.

Mzuka kibao: Ulianza mziki lini na kwa sasa unavibao vingapi?

Ari Loveness: Mziki nmeanza kitambo kidogo kama miaka mi nne lakin kujulikana ilikuwa last year 2017, kwa sasa nko na vibao vitatu na kibao cha kwanza kilinicho nitambulisha kinaitwa You are mine ambacho nlishikishwa na producer wangu Lameckboy Kenya, na vibao viwili nimefanya solo.

Mzuka kibao: Kwanin umekuwa hujaskika hio miaka ya nyuma labda shida ni nini hasa?

Ari Loveness: Kwakweli nimekuwa masomoni alaf pia sikuwa na support hasa pesa za kurekodi na producer mzuri, lakin kuna rafiki yangu na kama kakangu aitwa Simon Sims alinichukuwa akanipeleka kwa producer Lameckboy Kenya na producer akapenda kipaji changu akaanza kunipa support mpaka sasa hivi.

Mzuka kibao: Na unafanya mziki aina gani na je wazaz wako wanakupokeaje na je uko na mkataba na producer wako?

Ari Loveness: Mim kwa sasa nafanya inspiration na gospel, kuhusu wazazi wangu haikuwa rahisi lakin nashukuru sai wako sawa na wananipa support. Kuhusu producer nikama kakangu tulipojuana nkapata ni family, yani Lameckboy ni cousin yangu na nashukuru anani support na ndio niko na mkataba nae pia yeye ndio manager wangu.

Mzuka kibao: Mashabiki watarajie nini kwa sasa baada ya kuachia wimbo wako wa mapigo ya moyo je kuna kitu kipya ama video labda?

Ari Loveness: Naam video ya mapigo ya moyo ipo ready nmefanya na director Flava Wa Flava Films, pia song mpya inakam na naomba wanpe support sana.

Mzuka kibao: Asante sana kwa mda wako, Neema ya Mungu ikuongoze.

Ari Loveness : Asante sana kwa interview, Mungu akusaidie pamoja na team nzima ya Mzuka Kibao.

Mzuka kibao: Amen

DOWNLOAD ¦ Ari Loveness – Mapigo Ya Moyo (Prod by Lameckboy)

Searching - 2Baba (aka 2Face Idibia) feat. Bongos Ikwue Macvoice Ft. Leon Lee & Rayvanny – Pombe 🎵 🎶 🎹 🎼 🍗 💃 🎸

SONG OF THE WEEK

MANIFEST - King Kaka (Rabbit) feat Nviiri The Storyteller Joeboy - Alcohol Joeboy - Show me ️💯💯

️💯💯

FOR FAST LATEST UPDATES ON

AUDIOS, VIDEOS, MIXTAPES, FREE BEATS AND INSTRUMENTALS

CLICK HERE TO JOIN OUR WHATSAPP GROUP

🎵🎶🎹🎼🍗 💃 🎸🎧🔉 Mercy-Chinwo-Onememma Lucky-Dube-Remember-Me Omah-Lay-Understand Guchi-Jennifer Chike-Running-To-You-ft-Simi Lucky-Dube-Prisoner AZAWI-Majje-ft-Fik-Fameica Kidi-Touch-It Nandy-Nimekuzoea Guchi-Jennifer-Remix-ft-Rayvanny

MZUKA KIBAO TELEGRAM CHANNEL

SUBSCRIBE TO STAY UPDATED

🎵🎵🎶🎵🎵🎤🎵🎵🎹

🎵 🎶 🎹 🎼 🍗 💃 🎸

Woman - Simi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here